WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA

Watumishi wa Umma wametakiwa kuchangamkia nyumba zinazojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Nyumba Tanzania (TBA), ili kupata makazi bora baada ya kustaafu.
Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Josephat Asunga wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa nyumba zinazojengwa na TBA jijini Dar es Salaam jana.
“Nawaomba watumishi wa umma kuzichangamkia nyumba hizi ambazo kwa  wao wanafursa ya kukopeshwa na kulipa deni polepole” amesema Asunga.
Amesema kuwa nyumba hizo zimejengwa na kuwekewa miundombinu mizuri hivyo kuwa ni sehemu bora ya kuishi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wakala wa Nyumba Tanzania (TBA), Mhandisi Elius Mwakalinga amesema nyumba zinazojengwa na TBA bei yake ni ndogo ukilinganisha na zile zinazojengwa na watu wengine.
“Hapa kwetu bei ya nyumba inaanzia sh.milioni 35 hadi milioni 200 wakati  maeneo mengine ni kuanzia sh.milioni 600” amesema Mwakalinga.
Aidha, amesema kuwa katika awamu ya tatu ya mradi TBA walipata mkopo wa sh.Bilioni 25 ambapo hadi Februari 2017 walipata mkopo wa sh.Bilioni 19.5 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuwauzia watumishi wa umma.
 Hata hivyo, amesema kuwa changamoto kubwa katika mradi huo ni watu kujenga nyumba katika baadhi ya viwanja ndani ya eneo la mradi hivyo kupunguza idadi ya nyumba zilizokusudiwa kujengwa katika hatua za awali za awamu ya tatu ya mradi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post