WAZIRI MWAKYEMBE AELEZA ILIPOFIKIA RIPOTI YA NAPE KUHUSU RC MAKONDA KUVAMIA CLOUDS

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe leo amefanya mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma na kuzungumzia mikakati ya wizara yake katika kuhakikisha tasnia ya sanaa, utumaduni na michezo inazidi kukua zaidi nchini katika kipindi cha uongozi wake.
Waziri Mwakyembe alieleza mambo mengi wakati wa mkutano huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa jithada za makusudi zinafanyika kuweza kukuza lugha ya kiswahili huku akiwasihi watanzania kujisikia fahari kuzungumza lugha hiyo popote pale wanapokuwa.
Mimi nimekaa Ujerumani, kule wanakulazimisha kuijua lugha yao kwani ndiyo inayotumika zaidi. Hapa kwetu Rais ametuonyesha mfano nadhani sasa na sisi tufuate kukuza lugha hii, alisema Waziri.
Waziri Mwakyembe pia alizungumzia suala la kuhakikisha Serengeti Boys inafanya vizuri Gabon na hata kwenda kombe la dunia kwani ni heshima kubwa kwa  taifa.
Akijibu swali lwa mwandishi wa habari kuhusu alipofikia na ripoti ya aliyekuwa Waziri, Nape Nnauye kuhusu madai ya RC Makonda kuvamia ofisi za Clouds Media, Waziri Mwakyembe alisema kuwa yeye hajapokea ripoti hiyo, na hata akiipokea hawezi kuiwasilisha popote sababu haijakamilika.
“Mimi hiyo ripoti sijaiona na kama mwanasheria kwangu ni mwiko na sitapeleka taarifa ambayo haijakamilika. Kupitia vyombo vya habari taarifa imeeleza kuwa ushahidi ulitolewa na upande wa Clouds Media Group na mkakiri kuwa upande wa pili haukupatikana. Huwezi kuwa Hakimu kwenye suala lako wewe mwenyewe, kufanya hivyo ni ubatili kwahiyo hata mimi ningekuwa ni mwandishi wa habari ningesema hili jambo siliwezi kwakuwa linanihusu na mimi.”
Baada ya kusema hayo aliendelea kufafanua kuwa, suala hilo atalifanyika kazi kwani anataka kuhakikisha kunakuwapo na uhuru wa habari lakini yeye hatoliundika kamati.
“Mimi sikuapa kwa jambo hilo moja pekee lakini mimi ni mwanasheria mkongwe na nitahakikisha nalifuatilia lakini mimi sitaunda kamati katika jambo hilo.”
Ripoti iliyowasilishwa kwa aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Nape Nnauye ilieleza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia kituo cha Clouds usiku akiwa na Askari wenye silaha akilazimisha video ya mwanamke anayedai kuzaa na Askofu Gwajima kurushwa hewani.
Kuhusu kumhoji Makonda, kamati hiyo ilisema kuwa kiongozi huyo kwa hiari yake mwenyewe alikataa kuhojiwa baada ya kuwatoroka wanakamati wwaliokwenda ofisini kwake kumhoji.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post