WEMA SEPETU AKWAMA MAHAKAMANI KESI YA DAWA ZA KULEVYA

Kesi ya Dawa za kulevya inayomkabili muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu iliyokuwa isikilizwe leo, imeahirishwa hadi Aprili 11 mwaka huu baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi haujakamilika.
Wema Sepetu alishtakiwa baada ya kukutwa na msokoto wa bangi pamoja na karatasi maalum za kuvutia dawa hiyo, jeshi la polisi lilipofanya upekuzi nyumbani kwake mapema mwezi uliopita.
Muigizaji huyo ni miongoni mwa wasanii na watu maarufu wengi waliotajwa katika orodha ya watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Orodha hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post