YANGA YATAMBA KUIFUNGA AZAM FC VPL

Uongozi wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam,umesema kwamba kwa sasa nguvu zao wanazielekeza kwenye michezo yao ya ligi kuu ya Tanzania bara iliyosalia ukiwemo mchezo wao dhidi ya Azam FC utakaopigwa siku ya tarehe moja ya mwezi wa nne mwaka huu.

Katibu mkuu wa Yanga Charse Boniphace Mkwasa,amesema kuwa baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhdi ya Zanaco  kwa sasa nguvu zao zote zinaelekezwa kwenye ligi.

Mkwasa amesema kwamba kwa sasa wanasubiri lipoti ya kocha mkuu kufahamu progarm zake za mazoezi hii inatokana na timu hiyo kurejea hapo jana wakitokea nchini Zambia walipokwenda kushiriki mchezo wa kimtaifa dhidi ya Zanaco.

Alisema kwamba hata ratiba ya ushiriki wao kwenye shirikisho walipoangukia wanategemea kupata taarifa lipoti hiyo ya kocha George Lwandamina kuhusu mipango yake.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post