ZLATAN IBRAHIMOVIC AIPA MASHARTI MAN UTD

Mshambuliaji wa Man Utd Zlatan Ibrahimovic ameripotiwa kuwa katika mpango wa kutaka kusalia Old Trafford kwa miaka mingine miwili.
Gazeti la The Daily Mirror limechomoza mapema hii leo na taarifa hiyo, ikiwa ni siku tatu baada ya meneja wa Man Utd Jose Mourinho akisisitiza mshambuliaji huyo kubaki klabuni hapo.
Ibrahimovic amesaliwa na miezi mitatu kabla mkataba wake wa mwaka mmoja na Man Utd haujafikia kikomo, na tayari mazungumzo ya awali yameanza kuchukua nafasi yake huko Old Trafford.
Taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la The Daily Mirror zimedai uchunguzi wa ndani ambao umefanywa na mwandishi wa habari hizi, zinasema Zlatan huenda akakubali kubaki Man utd kwa miaka miwili.
Hata hivyo alipoulizwa na waandishi wa habari mapema juma hili alisema suala la mkataba mpya linapaswa kusubiri hadi mwishoni mwa msimu huu, ambapo atakua amemaliza majukumu ya kuipigania Man Utd ili ifikie malengo yake.
Taarifa nyingine zilizochapishwa na gazeti la The Mirror zimedai kuwa, Zlatan ameupa masharti uongozi wa Man Utd kwa kuutaka umlipe mshahara wa Pauni 300,000 kwa juma, endapo unahitaji aendelee kubaki klabuni hapo kwa kipindi kingine.
Endapo mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za Barcelona, AC Milan, Juventus, Inter Milan na PSG atakubali kusaini mkataba mpya na Man Utd, atacheza ligi ya England akiwa na umri wa miaka 37.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post