ALEXIS SANCHEZ AIPELEKA ARSENAL FAINALI YA FA

Goli la muda wa ziada lililofungwa na Alexis Sanchez limeipeleka Arsenal katika fainali ya FA kuvaana na Chelsea baada ya jana kuifunga Manchester City magoli 2-1.

Sanchez aliivusha fainali Arsenal katika dakika ya 11 ya muda wa ziada baada ya mabeki wa Manchester City kushindwa kuzuia mpira wa adhabu wa Mesut Ozil.

Arsenal walionekana kupambana kiume wakitokea nyuma baada ya Sergio Aguero kufunga goli katika dakika ya 62, lakini Alex Oxlade-Chamberlain akasawazisha goli hilo dakika 11 baadaye.
                                        Sergio Aguero akifunga goli la kwanza katika mchezo huo 
                     Alexis Sanchez akifunga goli lililoipeleka Arsenal katika fainali ya FA
Sio Mieleka: Olivier Giroud na Vincent Kompany wakianguka chini wakati wakichuana kuwania mpira 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post