ALIYETUMBULIWA NA RAIS MAGUFULI APATA KAZI UMOJA WA MATAIFA (UN)

Dkt. Mwele Malecela ameteuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa Mkurugenzi Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kupambana na Magonjwa (Director of Africa Centers for Diseases Control and Prevention) ambapo atakuwa akifanyika kazi Brazzavile, Congo.
Dkt. Mwele alikuwa ndiye mwanamke wa kwanza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ya nchini Tanzania kabla ya Rais Dkt Magufuli hajatengua uteuzi wake mapema tarehe 16 Desemba, 2016.
Rais Dkt Magufuli alitengua uteuzi huo baada ya Dkt Mwele kunukuliwa tarehe 15 Disemba 2016 akisema kuwa, Tanzania kuna uwepo wa ugonjwa wa Zika na kwamba asilimia 15 ya waliopimwa walikutwa na virusi vya ugonjwa huo ambapo hata hivyo taarifa hizo zilikanushwa na wizara ya afya leo.
Taarifa za kuwepo virusi vya Zika nchini zilikanushwa na Wizara ya Afya ambapo Naibu Waziri Dkt Hamis Kigwangalla alisema kuwa utafiti uliofanyika si wa kuchunguza Zika bali ni kuangalia kama vipimo vilivyopo vinaweza kutumia kupima ugonjwa huo.
Profesa Yunus Mgaya Mkurugenzi NMRI
Disemba 17, 2016 Rais Magufuli alimteua Profesa Yunus Mgaya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu  (NIMR) akichukua nafasi ya Dkt Mwele.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post