ANTONIO CONTE ACHEKELEA KUIFUNGA MAN CITY

Kocha wa Chelsea Antonio Conte amesema timu yake imepiga hatua kubwa ya kuelekea kutwaa ubingwa wa ligi kuu England badaa ya kuifunga Manchester City usiku wa kuamkia Leo magoli 2-1
Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Stanford Bridge, Eden Hazard ameifingia Chelsea magoli yote mawili, huku goli la Man City likifungwa na Sergio kun Aguero.
Conte anasema ni ushindi muhimu Kwani ameupata dhidi ya  timu ngumu, hasa ukizingatia wiki iliyopita amepoteza mchezo dhidi ya Crystal Palace.
Conte ameongeza kuwa ushindi huo ni hatua kubwa ya kuelekea kutwaa kombe la England lakini bado anamichezo nane mkononi na anahitaji point 18 kijihakikishia ubingwa huo.
Chelsea Sasa imefikisha point 72 na kuicha Tottenham nyuma kwa point 7.
Kwa upande wake kocha wa Manchester City Pep Guadiola amesema, baada ya kufungwaa jana na Chelsea amejitoa rasmi kwenye kinyangiro cha ubingwa.
Guadiola amesema sasa anapambana kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Klabu bingwa Ulaya na habari za ubingwa hazipo tena kichwani mwake.
Kipigo dhidi ya Chelsea ni Kipigo cha sita kwenye ligi kuu England na hii ni mara ya kwanza kwa Pep kupoteza mechi sita ndani ya ligi kuu tangu aanze  kufundisha Barcelona na baaadae Buyern Munich.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post