ASILI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAJINGA DUNIANI (APRILI MOSI)

Siku ya wajinga duniani, ni siku ambayo huadhimishwa kila mwaka mwezi Apili Mosi. Siku hii hutumiwa na watu wengi na hata baadhi ya taasisi kubwa kufanyiana utani.
Watu wanaofanyiana utani katika siku hii, huishia kwa kuwaambia wale waliowatania ‘Leo ni siku ya wajinga’.
Baadhi ya magazeti na majarida mbalimbali huandika habari ambazo si za kweli, kwa lengo la kuwatania watu, na mwisho wa habari hiyo huandika kuwa si ya kweli bali ni kuadhimisha siku ya wajinga au kutoa taarifa nyingine ya kuikanusha habari hiyo katika gazeti linalofuatia.
Kwa mujibu wa gazeti la washington Post, asili ya siku ya wajinga ilianza mwaka 1582 wakati ambapo ufaransa ilibadili kalenda ya Julian na kuhamia kwenye kalenda ya Gregorian.
Mabadiliko haya ya kalenda yalibadilisha tarehe za mwaka na hivyo nchi ikaanza kusherehekea mwaka mpya Januari Mosi badala ya Aprili.
Mabadiliko hayo ya kalenda yaliyofanywa na Papa Gregory wa 13, hayakuwafikia wananchi wote wa Ufaransa. Badala yake baadhi waliendelea kusherehekea mwaka mpya Aprili Mosi. Watu hao walionekana kama wajinga na siku hiyo ikaitwa ni siku ya wajinga.
Wapo walioihusisha siku hii na sherehe za Warumi zilizokuwa zikiadhimishwa Aprili Mosi, ambapo watu walivaa nguo za ajabu ajabu na za kuchekesha. Sherehe hizo zilikuwa zikianza Machi 25 na kuisha Aprili Mosi.
Baadhi ya wanahistoria wa Uingereza waliihusisha siku hii na sherehe zinazifanywa kila Aprili Mosi nchini India ambapo watu hurushiana vitu na kuchafuana kwa rangi au vyakula kama sehemu ya utani.
Kama ilivyo siku ya mazingira duniani, baadhi ya taasisi kubwa duniani huadhimisha siku ya wajinga na kuwaweka mtegoni maelfu ya watu.
Mnamo mwaka 2008 televisheni ya Uingereza BBC ilionyesha kipande kifupi cha video katika kipindi cha Panorama kilichoonyesha wakulima huko Uswisi wakivuna tambi (Spagetti). Dakika chache baadaye mamia ya wananchi wa Uingereza walijaa katika ofisi za shirika hilo la habari wakitaka kujua aina hiyo ya kilimo cha tambi.
Duka kubwa la vyakula (supermarket) la nchini Uingereza liliweka tangazo kuwa limetengeneza karoti zinazoweza kupiga mluzi wakati wa kuzipika. Wateja wengi walimiminika na kwenda kuzinunua.
Hapa nchini mwaka 2006 gazeti moja liliwahi kutoa tangazo la kuwataka wasichana wote mabikira kufika katika ofisi za gazeti hilo ili wapate ajira. Mamia ya wasichana walifurika asubuhi ya siku hiyo katika ofisi za gazeti hilo.
Ila ibainike kuwa siku hii siyo siyo sikukuu ya kitaifa katika nchi yoyote duniani. Baadhi ya watu wamekuwa wakiipinga siku hiyo na wengine kuikubali kuwa haina tatizo lolote.
Badhi ya viongozi wa dini wamesema kuwa siku hiyo haijabainishwa katika biblia, hivyo si vyema kuisemea moja kwa moja kama inafa ama haifai, ila wameshauri watu kufuata dhamira zao zinavyowaongoza.
Japo viongozi wengine wa dini ya Kiislamu wako kinyume na wale wa mwanzo kwa kusema kuwa, katika Quran takatifu, uongo wa aina yoyote ni dhambi, iwe ni uongo wa utani ama wa kweli, ni dhambi kusema uongo. Hivyo hawakubaliani na maadhimisho ya siku hiyo.
Siku hii ni siku inayofurahisha na kuburudisha hasa pale unapoweza kuwadanganya marafiki zako au wafanyakazi wenzako kazini na wakadanganyika.
Ila pia siku hii inaweza kuwa na madhara mbali mbali katika jamii, ikiwemo mshtuko na fedheha kwa baadhi ya watu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post