ASKOFU GWAJIMA ASHINDANA NA RAIS MAGUFULI KUHUSU KUNUNUA TRENI ZA UMEME

Yakiwa ni takribani majuma mawili sasa tangu Rais Dkt John Pombe Magufuli alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), Pugu jijini Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ameweka wazi mpango wake wa kununua treni ya umeme ili iawasaidie waumini wake katika safari.
Alisema kuwa treni hiyo itatumika siku za ibada kubeba waumini huku wakiimba nyimbo za kumtukuza Mungu. Lakini pia alisema atakuwa tayari kuruhusu itumike kubeba abiria wa kawaida.
Askofu Gwajima aliyasema hayo jana kanisani kwake, ambapo alieleza gharama za treni hiyo ni TZS bilioni 11 lakini hakusema ni lini hasa atainunua.
“Siku moja nilimchukua mwalimu Bihagaze, alikuwa mwalimu wangu wa Biblia, nikamwambia twende nikakuonyeshe mji wa mwanakondoo, nikamchukua na helkopta hadi shambani ambapo ni mji utakuwa na mahoteli, universities, kituo cha mafuta na kila kitu,”  alisema.
Alifafanua kuwa katika mji huo, kuna ramani inaonyesha kuwa reli inapita katikati. “Alipopaona akasema mbona kuna reli inapita katikati, nikamwambia nitanunua treni, akashangaa akaniuliza, treni ni shilingi ngapi? Nikamwambia dola milioni nne na mabehewa yake dola milioni tano hivi, akasema nikulipie? Nikamwambia nitanunua mwenyewe. Akapiga magoti kusujudu nikamwambia yapo mengi yanakuja,” alisema Askofu Gwajima huku waumini wake wakimshangilia kwa shangwe.
Ujenzi wa reli uliozinduliwa na Rais Dkt Magufuli Aprili 12 mwaka huu, utakamilika ndani ya miezi 30, ambapo kwa awamu ya kwanza utaanzia Dar es Salaam hadi Morogoro, treni ikiwa na uwezo wa kukimbia umbali wa 160km/hr. Treni itakuwa na jumla ya mabehewa 100.
Chanzo: Mwananchi
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post