ASKOFU GWAJIMA ATISHIWA KUUAWA

SHARE:

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema ametishiwa kifo na kundi la watu asiowafahamu. Amesema kuwa watu hao wali...

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema ametishiwa kifo na kundi la watu asiowafahamu.
Amesema kuwa watu hao waliomtumia ujumbe wa maandishi (SMS) kupitia simu yake ya mkononi na kuusambaza kwa watu, wengine walidai hatomaliza wiki hii iliyoanza leo.
Jana katika ibada yake, Gwajima alisema kuwa baada ya kuupata ujumbe huo alifanya maombi kwa ajili ya kuwafuta waliomtumia  na kujua nini chanzo cha vitisho hivyo.
“Kuna Askofu anajiita Nabii mdogo juzi alikuwa anasambaza meseji anasema naona Gwajima anamaliza mwendo wake, nimeapa kwa jina la bwana yeye anayesema nitamaliza mwendo kwa nguvu za giza atamaliza yeye kwanza na siyo mimi” alisema Gwajima
Aliongeza kuwa chombo cha Mungu hakiwezi kwenda mbinguni kabla hakijamaliza kazi ya Mungu na kwamba ataendelea kuishi hadi pale Mungu atakapoona imetosha na siyo kwa vitisho vya binadamu.
“Jana nilikuwa namsaka aliyetuma meseji hiyo kwenye makorido ya kiroho, nikamuona, mimi nina agano na Bwana kwamba adui zangu wakija kwa njia moja wataondoka kwa njia saba, silaha zote zitakazokuja kwangu hazitofanikiwa, yeye ndiye atakayekufa siku ile ile aliyoipanga, siyo mimi” alisema.
Alisema anawajua waliojiandaa kufanya uovu huo dhidi yake na kwamba haogopi chochote, kwani yeye ni sauti ya Mungu na ataendelea kufanya kazi kwa nguvu kama alivyoagizwa na Mungu ili kutimiza kusudi lake hapa duniani.
“Unasema Gwajima atakufa, najua mipango yako yote, nawajua wale watu uliowaandaa kwa ajili ya kuuwa wapo wapi, wana umri gani na wanafanya kazi gani. Huyu anachekesha  kweli, unataka Mungu akose sauti yake, watakufa wao waliotumwa na siyo mimi”
Gwajima alisema kuwa yeye na waumini wake wataendelea kuwa imara kwani wanamjua wanayemwamini na hawatishiwi na vitisho vya kifo kwa sababu Mungu atawashindia.
alinukuu maneno katika Biblia na kusema “Nimepewa uwezo wa kuianza kazi hadi niimalize, mimi nina agano la bwana kwamba amwaminie yeye ataishi, na mimi nasema sintakufa bali nitaishi ili niyasimulie matendo makuu ya Mungu, sintaogopa silaha ya mchawi, iwe panga, iwe risasi haitofanikiwa mimi nitaishinda hadi niimalize kazi yangu.” 
Askofu huyo amekuwa katika vita ya maneno na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam tokea alipotajwa  katika sakata la orodha ya watuhumiwa wanaojihusisha na ama uuzaji au utumizi wa dawa za kulevya. Hata hivyo, Gwajima alijisalimisha polisi akapimwa na kubainika kuwa hajawahi kutumia dawa hizo na hivyo kuachiwa huru.
Vita hiyo ya maneno haikuishia hapo mpaka pale kiongozi huyo wa Mkoa wa Dar es salaam alipovamia kituo cha habari cha Clouds kulazimisha habari ya mwanamke aliyehojiwa akisema amezaa na Gwajima irushwe hewani ili kumchafua Askofu huyo wa kiroho.
Tukio la kuvamiwa kwa kituo cha Clouds lililoundiwa kamati ya uchunguzi na aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye lilipelekea kutupwa nje kutokana na mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Dkt Magufuli, ambapo aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi hiyo ya Nape ili kuiongoza Wizara hiyo.
HT @ TanzaniaDaima

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: ASKOFU GWAJIMA ATISHIWA KUUAWA
ASKOFU GWAJIMA ATISHIWA KUUAWA
https://1.bp.blogspot.com/-Jc8hFlPA5No/WOIVpiVQTbI/AAAAAAAAZC8/_z18S0uTOjoGD9SAeqxP0fSN_PyWmBP5wCLcB/s1600/xd640b__GWAJIMA22B1-640x375.jpg.pagespeed.ic.K9LtQ6Gdqr.webp
https://1.bp.blogspot.com/-Jc8hFlPA5No/WOIVpiVQTbI/AAAAAAAAZC8/_z18S0uTOjoGD9SAeqxP0fSN_PyWmBP5wCLcB/s72-c/xd640b__GWAJIMA22B1-640x375.jpg.pagespeed.ic.K9LtQ6Gdqr.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/04/askofu-gwajima-atishiwa-kuuawa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/04/askofu-gwajima-atishiwa-kuuawa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy