AUAWA KWA RISASI BAADA YA KUVAMIA IKULU KENYA

Walinzi wa Raisi wamemfyatulia risasi na kumuua mtu aliyevamia eneo la Ikulu kwa kuruka uzio jumapili iliyopita ya tarehe 26 Machi wakati Rais Uhuru Kenyatta alipohudhuria mashindano ya mchezo wa golf huko Muthaiga.
Katika tukio hilo lililobakia kuwa siri huku uchunguzi ukiendelea, mtu huyo mwenye umri wa kati alisemekana kuingia katika eneo lenye ulinzi mkali muda wa saa 11 jioni na alikuwa katika egesho la magari lililopo karibu kabisa na nyumba ya Rais wakati alipoonekana na maafisa wa Elite General Service Unit wanaolinda eneo hilo.
Vyanzo mbalimbali vimesema kwa kujiamini kuwa maafisa wa ulinzi wa eneo hilo wanaamini mtu huyo aliruka uzio kwani si rahisi kwa yeyote kufika eneo alilokuwepo kupitia milango yote iliyopo pasipo kubainika.
Hii ni mara ya kwanza kwa mtu kupigwa risasi ndani ya eneo la ikulu kati ya matukio matatu yaliyowahi kuripotiwa watu kuvamia ikulu tokea Rais Kentatta alipohamia katika ikulu hiyo mwaka 2013.
Chanzo kimoja kilisema kuwa mtu huyo baada ya kupigwa risasi na kufariki alikutwa na kisu lakini hakuwa na silaha nyingene yoyote.
Mwili huo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Jiji na mpaka kufikia Ijumaa hakuna mtu yeyote aliyejitokeza kuuchukua.
Msemaji mkuu wa Ikulu, Manoah Esipisu alisema kuwa hawezi kuzungumzia tukio hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Joseph Boinnet, Mkuu wa kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai Ndegwa Muhoro pamoja na Kamanda wa Kaunti ya Nairobi, Japheth Koome walipotafutwa hawakupatikana ili kuzungumzia tukio hilo.
Afisa mmoja wa serikali ambaye alikataa jina lake kutajwa, alisema kuwa ripoti kuhusu tukio hilo bado haijakamilika ili kuwekwa wazi.
“Sina ripoti kamili ya tukio hili, polisi watakuwa wana maelezo mazuri zaidi” alisema huku akiongeza kuwa Msemaji Mkuu wa Ikulu hajaweka wazi chochote kwa kuwa tukio hili ni nyeti.
Aidha eneo hilo la ikulu ambalo liko katika marekebisho lilikaguliwa na hakukupatikana hatari yoyote kwa Rais wala familia yake.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post