BAADA YA MVUTANO, VIONGOZI WA UVCCM WATOLEA UFAFANUZI UTEUZI WA JOKATE MWEGELO

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) hivi karibuni umemteua mjasiriamali Jokate Mwegelo kuwa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM Taifa.
Uteuzi wa Jokate Mwegelo ambaye pia amewahi kushinda katika Shindano la Miss Tanzania na kushika nafsi ya pili mwaka 2006 umeonekana kuwagawa viongozi wa jumuiya hiyo huku baadhi wakiamini kuwa uteuzi huo haukufuata kanuni na taratibu zinazotakiwa.
Baadhi ya taarifa zinazodaiwa kutokana ndani ya jumuiya hiyo, zinadai kuwa baadhi ya viongozi wanalalamika kwamba hawakuhusishwa kwenye uteuzi huo.
Kufuatia taarifa mbalimbali kusambaa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na baadhi ya vyombo vya habari, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka amezungumza na vyombo vya habari na kulitolea ufafanuzi suala hilo.
Shaka amesema kuwa ni kweli anafahamu Jokate kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo na kwamba uteuzi huo ulifuata taratibu zote za chama zinazotakiwa.
“Ni kweli amekaimishwa kwa kufuata taratibu zote za chama. Kikao cha Kamati ya Utekelezaji kilikutana Aprili 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam na ndicho kimewakaimisha wakuu wa idara watano akiwemo Jokate,”  alisema Shaka.
Shaka amesema yeye ni mjumbe wa kikao hicho na kazi yake kubwa ni kuhakikisha kwamba hakuna kanuni inayovunjwa wakati wa utendaji kazi. Pia alifafanua kuwa mabadiliko yaliyofanywa katika Katiba ya CCM sasa yanaruhusu Baraza Kuu kukutana mara mbili kwa mwaka (kila baada ya miezi 6), sasa hatuwezi kukaa na nafasi iko wazi hadi Baraza Kuu litakapokutana. Kamati ya Utekelezaji ina mamlaka ya kukaimisha wakuu wa Idara kisha Baraza Kuu likikutana ndio litathibitisha, alisema Shaka.
Jokate kwa upande wake yeye aliishukuru kamati husika kwa kumteua katika nafasi hiyo, huku akisema kuwa atatumia uwezo wake wote kufanya kazi kwani hilo ni deni kubwa kwake.
“Naishukuru Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM TAIFA kwa kuonyesha mapenzi makubwa na imani kubwa kwangu kwa kukubali kuniteua ku-kaimu nafasi ya Katibu wa UHamasa na Chipukizi. Imani yenu kwangu inabaki kuwa deni na chachu ya kujitoa kwa nguvu zote, kwa akili zote kuitumikia vizuri nafasi hii. Mwenyezi Mungu anisaidie.”
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post