BAADA YA SAKATA LA MADAWA MASOGANGE AWADILITI MASHOSTI

SIKU chache baada ya kufi kishwa mahakamani kwa msala wa madawa ya kulevya, mrembo ambaye alitengeneza ustaa wake kupitia Video Queen Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa hataki kabisa kujichanganya na mtu yeyote kwenye kipindi hiki badala yake ameamua kujituliza na hata marafi ki wengi anawapunguza.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Masogange alisema kuwa hakuna kitu kizuri maishani kama kuamua kupunguza vitu vingine ambavyo vilikuwa havina umuhimu wowote maishani na pia hata marafi ki wengine ambao alikuwa nao, hawakuwa wakimuongezea chochote zaidi ya majanga.

“Maisha yangu nimeyabadili kwa kiasi kikubwa sana kuna vitu vingi sana nimeviondoa ili tu niweze kubadilisha mfumo wangu niliouzoea huko nyuma, sasa hivi naona niko vizuri tu baada ya vitu ambavyo siyo muhimu kwangu kuviweka kando,” alisema Masogange.

Februari mwaka huu, Masogange alifi kishwa katika Mahakama wa Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka ya kutumia madawa ya kulevya kisha akatoka kwa dhamana na kesi yake inaendelea mahakamani hapo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post