BALOZI SEIF AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUTANGULIZA UZALENDO WAWAPO KAZINI

SHARE:

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Cheti Maalum Mama Asha Suleiman Iddi aliyekuwa Katibu Muhtasi wa Wazi...

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Cheti Maalum Mama Asha Suleiman Iddi aliyekuwa Katibu Muhtasi wa Waziri Kiongozi ambae amefikia umri wa Kustaafu Utumishi wa Umma hapo Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawailishi.
Mstaafu wa Idara ya Upigaji chapa Bibi Kiboga Suleiman Mohamed akipokea cheti Maalum kutoka kwa Balozi Seif baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi wa Umma Serikalini.
Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mstaafu Bwana Abdulla Ali Abdulla Kitole akipokea zawadi ya Laptop kutoka kwa Bosi wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kama ukumbusho akiwa katika mapumziko yake ya ustaafu Serikalini.
Mhasibu Mkuu Mstaafu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Makame Mussa Sururu akikabidhiwa zawadi yake ya Jokovu la kuhifadhia vitu baridi kutoka kwa Balozi Seif kwenye hafla ya kuagwa kwao rasmi baada ya kumaliza muda wao wa Utumishi Serikalini.
Balozi Seif kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Wizara ya Nchini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pamoja na wafanyakazi wastaafu wa Ofisi hiyo walioagwa rasmi hapo Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni.

Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wake Mh. Mohamed Aboud Mohamed, Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi ambae ni Mstaafu na Mkurugenzi Uendeshaji wa Ofisi hiyo Bibi Halima Ramadhan Toufiq. 
 

Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wake Mh. Mihayo Juma N’hunga, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Ng. Joseph Abdulla Meza na Naibu wake Nd. Ahmad Kassim Haji.  Picha na – OMPR – ZNZ.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Wafanyakazi wanapaswa kujitahidi kutekeleza majukumu yao ya Utumishi wa Umma kwa kufanya kazi kizalendo na ushirikiano uliotukuka ili kujijengea mazingira bora ya hatma yao ya baadae.

Alisema tabia hiyo njema itawapa heshima kubwa katika Jamii kiasi wamba wamalizapo muda wao wa Utumishi watajikuta wakiacha athari inayoendelea kukumbukwa kwa wema na watumishi wenzao waliowaacha.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa hafla maalum ya kuwapongeza na kuwaaga Wafanyakazi 13 waliostaafu kati ya Mwaka 2015/2016 na 2016/2017 wa Idara tofauti zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Alisema haipendezi na ni hulka mbaya inayowakumba baadhi ya Watumishi wa Umma hawa wale wenye mardaraka pale wanapofikia muda wao wa kustaafu na walio nyuma yao wakasherehekea kwa Pilau kutokana na vitendo vyao vilivyokosa imani kwa kutowatendea haki.Balozi Seif aliwapongeza Wafanyakazi wote waliostafu kwa kumaliza Utumishi wao katika njia ya salama na afya njema iliyopatikana kwa wao kuzingatia na kufuata mashauri ya Kitaalamu ya Afya katika mfumo wa kufanya mazoezi baada ya muda wa kazi.

Aliwataka wafanyakazi wanaofikia umri wa kustaafu kuachana na tabia ya kujenga hofu kipindi wanachokaribia kumaliza muda wao wa Utumishi kwani kinaweza kuwasababishia msongo wa mawazo yanayoishia kupata maradhi.

Balozi Seif alitanabahisha wazi kwamba kustaafu sio mwisho wa maisha lakini kinachotakiwa kwa wastaafu hao ni kujipanga vyema ili kukabiliana na mabadiliko ya maisha mapywa wanayoyaingia.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka wafanyakazi wapya na wale wanaoendelea na utumishi wao kutumia maarifa, uzoefu, ujuzi na hata mbinu zilizokuwa zikitumiwa na watangulizi wao waliostaafu ili kupata ufanisi mzuri kwa Wizara na Taifa kwa ujumla.

Mapema akitoa Taarifa fupi ya wafanyakazi hao wastaafu, Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bibi Halima Ramadhan Toufiq alisema Utumishi wa Wafanyakazi hao wastaafu katika Taasisi za Umma umesaidia kizazi kipya katika kuendeleza gurudumu waliloliacha.

Bibi Halima alisema licha ya wastaafu hao kuwa na uwezo kamili wa kuwajibika zaidi lakini Kifungu cha 68 {1} cha Utumishi wa Umma kimeweka bayana kuhusu kumaliza kwa Mkataba wa ajira. 

Mkurugenzi huyo wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka wastaafu hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa wafanyakazi wapya ili kuwapa maarifa yatakayowasaidia kumudu vyema kutekeleza kazi zao.

Bibi Halima aliwataja Wafanyakazi hao 13 wastaafu kuwa ni pamoja na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi aliyekuwa Katibu Muhtasi wa Waziri Kiongozi na Ndugu Abdulla Ali Abdulla Kitole aliyekuwa Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Wengine aliowataja ni Nd. Khatib Said Khatib aliyekuwa Mkurugenzi Uratibu, Bibi Shinuna Idara ya Faradha, Nd. Makame Mussa, Nd. Hassan Mohamed Hassan , Nd. Tajo Hussein Mawele, Bibi Amina Hussein Haji, Maabad Mlekwa Maabad, Siende Khatib Khamis, Mafunda Khamis Hamad, Kiboga Suleiman na Aziza Khalef Mohamed.

Wastaafu hao pamoja na mambo mengine walikabidhiwa vyetu maalum, zawadi mbali mbali kulingana na kada zao pamoja na fedha taslim kama ni ukumbusho kwao kutokana na utumishi wao mzuri uliotukuka.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Wastaafu wenzake 13 Mstaafu nambari moja katika kundi hilo Mama Asha Suleiman Iddi alikiasa Kikazi kipya kinachoingia katika ajira mpya iwe ya Umma na hata ya Sekta binafsi kuacha tamaa ya kutaka kujilimbikizia mali na utajiri ndani ya kipindi kifupi cha ajira zao.

Mama Asha alisema kitendo hicho ambacho hushabikiwa na baadhi ya watu mitaani kwa kuonekana mjanja na mwenye maarifa mbali ya kuhatarisha ajira zao laikini pia kinakwenda kinyume na kanuni, maadili na heshima ya Kazi.

Akizungumzia suala na viinua mgongo vya watumishi wastaafu Mama Asha aliziomba Taasisi zinazosimamia masuala hayo kufanya juhudi za ziada katika kuona haki za wastaafu hao zinapatikana kwa wakati muwafaka bila ya kuleta kughdha yoyote.

Alisema zipo dalili zinazoonyesha kuwatia hofu baadhi ya watumishi wastaafu kutokana na kucheleweshewa masurufu yao ambayo tayari wameshalenga kuwaendelesha katika muda wao wa kumalizia maisha.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: BALOZI SEIF AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUTANGULIZA UZALENDO WAWAPO KAZINI
BALOZI SEIF AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUTANGULIZA UZALENDO WAWAPO KAZINI
https://1.bp.blogspot.com/-3d6PBVWINPw/WPisSD_9ftI/AAAAAAAAZvw/er9jQpRCgTkZ3fLAOsLSjFziO1V9geNBACLcB/s1600/215.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-3d6PBVWINPw/WPisSD_9ftI/AAAAAAAAZvw/er9jQpRCgTkZ3fLAOsLSjFziO1V9geNBACLcB/s72-c/215.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/04/balozi-seif-awataka-watumishi-wa-umma.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/04/balozi-seif-awataka-watumishi-wa-umma.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy