BANGI KUHALALISHWA NCHINI KENYA

Nchi jirani ya Kenya ipo mbioni kuhalalisha matumizi ya Bangi kwa wananchi wake kutoka na zaidi ya Wakenya 1,400 kuuunga mkono ombi la kutaka kuidhinishwa kwa matumizi ya mmea huo baada kuwasilishwa kwa hoja hiyo mbele ya bunge la seneti na mtafiti Gwada Ogot.
Iwapo ombi hilo la mtafiti Gwada Ogot litaidhinishwa haitakuwa haramu kupanda ama hata kuuza bangi nchini Kenya. Gwada Ogot anasema kwamba matumizi ya kiafya pamoja na utumizi wa mmea huo viwandani unaojulikana kwa jina la sayansi kama Cannabis sativa una faida nyingi.
Anasema kuwa matumizi ya mmea huo yataimarisha hali ya uchumi nchini humo. Sheria ya Kenya inapiga marufuku utumizi wowote wa bangi na kwamba mtu yeyote atakayepatikana akitumia dawa hiyo atashtakiwa kwa uhalifu.
Ogot anaomba bangi kuondolewa miongoni mwa orodha ya vitu haramu na kutaka sheria mpya kuanzishwa ili kuweka bodi simamizi ya utumizi wa mmea huo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post