BARCELONA YATOTO MBELE YA MALAGA WAKATI NEYMAR AKITOLEWA

Neymar ametolewa nje ya uwanja wakati Barcelona wakipoteza mchezo wao dhidi ya Malaga kwa magoli 2-0 na kushindwa katika jitihada za kufikia pointi sawa na vinara wa Ligi ya La Liga Real Madrid.

Mabingwa hao watetezi wa La Liga walikuwa wamepata nafasi ya kuweza kufikia pointi za Real Madrid ambayo katika mchezo wa awali ililazimishwa sare ya 1-1 na Atletico Madrid.

Hata hivyo shambulizi la kipindi cha kwanza lililofanywa na mchezaji wa zamani wa Barcelona Sandro Ramirez na shambulizi la dakika za mwisho la Jony Rodriguez yalitosha kumaliaza Barcelona.

Katika mchezo huo mshambuliaji nyota Neymar alitolewa nje katika dakika ya 65, baada ya kupatiwa kadi ya pili ya njano. 
                                 Luis Surez akidhibitiwa na mabeki wa Malaga asilete madhara yoyote
                                    Jony Rodriguez akiifungia Malaga goli la pili na kuizamisha Barcelona
                                                       Neymar JR akionyeshwa kadi nyekundu na refa 

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post