BAYERN YACHUKUA TENA BUNDESLIGA

Ushindi wa mabao 6 kwa 0 waliopata dhidi ya Wolfsburg uliwafanya Bayern Munich kuchukua tena ubingwa wa ligi ya Ujerumani almaarufu kama Bundesliga.

Hii ilikuwa mara ya tano mfululizo kwa timu hiyo kutwaa kombe hilo kwani kuanzia mwaka 2013,2014,2015,2016 na mwaka huu Bayern wamebeba kombe hilo.

Hili ni kombe la kwanza kwa kocha Carlo Ancelotti toka ajiunge na Bayern msimu huu lakini linaweza kuwa la mwisho kwa kapteni wa timu hiyo Philip Lahm ambaye ameshashinda mataji 9 na timu hiyo.

Lahm alishatangaza nia yake ya kutundika daluga mara baada ya msimu huu kuisha na pia kiungo Xabi Alonso naye anaweza kufuata nyayo za Lahm mwishoni mwa msimu huu.

Wakati Bayern wakichukua ubingwa, huko nchini Hispania bado Real Madrid na Barcelona wanakimbizana kama kawaida kuwania ubingwa wa La Liga msimu huu.

Real Madrid waliibuka kidedea kwa kuibamiza Valencia mabao mawili kwa moja lakini baadae Luis Suarez alifunga mawili na Messi moja na kuifanya Barcelona kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao tatu zidi ya Espanyol.

Matokeo haya ya La Liga yanawafanya Barcelona  kuongoza msimamo wa ligi wakiwa na alama 81 sawa na Real Madrid lakini Barca anaongoza kwa tofauti ya mabao, Real Madrid ana mchezo mmoja mkononi ambao ndio unaweza kuwarudisha kileleni.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post