BIFU LA NAY WA MITEGO NA YUSUF MLELA SASA LIMEVUKA MPAKA

Wasanii wawili, mmoja kutoka Bongo Fleva na mwingine kutoka Bongo Muvi wamezidi kurushiniana maneno mitandao na vitisho vya kila namna kufuatia kutofautiana kwao juu ya suala la uingizwaji na usambazaji wa filamu za nje nchini Tanzania.
Nay wa Mitego ndiye alikuwa wakwanza kuwarushia madogo Bongo Muvi na kuwaita mataahira kutokana na kuandamana kwao kupinga uuzwaji wa filamu za nje nchini wakidai kuwa zanasababisha kudorora kwa soko la ndani. Baada ya maneno hayo, muigizaji Yusuf Mlela alimvaa Nay na kumwambia aache kutafuta kiki na kuwa si kila jambo lazima achangie.
Mlale alisema Nay kama anajiona yeye ni mbabe sana basi wapange pambano wapigane alafu wataona nani ni bingwa. Kufuatia kauli hiyo, Nay wa Mitego amemjibu kwa kumkejeli na kusema yeye amefunzwa vyema asipigane na wanawake.
“Nasikia kuna mwanaume/mwanamke yupo Bongo Muvi anataka kupigana na mimi, bahati mbaya mimi sipigani na mwanamke hata baba yangu aliniambia mwanamke hapigwi,” alisema Nay kupitia video iliyosambaa mtandaoni.
Aliongeza,“Naona kuna watu wanashadadia hili suala kwamba tupigane, mimi siwezi kupigana naye labda nitafutiwe mwanaume mwenzangu ili tutengeneze hela lakini kunipiganisha na mwanamke ambaye wamepoteza marinda hapana.”
“Baada ya kutangaza anataka kupigana na mimi, Bongo Muvi wenzake walinipigia simu wakaniambia achana na huyo mtu ni mwanamke mwenzao alishapoteza marinda,”
Baada ya maneno hayo ya kejeli, Mlela amerudi upya na kusisitiza bado anahitaji pambano na rapa huyo ili amshikishe adabu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mlema aliandika;
“Nay wa Mitego mimi nimelelewa vizuri na familia yangu ndio maana mambo ya matusi sijazoea ingawa nina uwezo mkubwa niliopewa na mungu baba wa kupambana na matamshi hayo. Kikubwa acha woga, kama shida yako ni pesa huyu aliyepoteza marinda si ndio itakuwa rahisi tu?. Kwangu mimi PESA SiO KILA KITU MUNGU NDIO KILA KITU. Nikuchape au nikuchape (uwezi) PESA ZOTE UTACHUKUA WEWE MIMI SIITAJI ATA SHILINGI MIA.”
Aidha, aliendelea kuandika, “Nay APA RINDA LIPO tena LA ZIGIZAGA uliza vizuri sio Kwa niliowatumia kama dustbin kupitisha siku….sitobishana na wewe tena coz akili yako ya kutaka sifa ni fupi.. eti unakataa movie wakati wewe mwenyewe unafanya movie au ujui kama izo video zako ni movie na TAIFA likiwa na utaratibu mzuri wa kazi za wasanii pia utafaidika…Acha maneno NJOO kwenye stage ili tuheshimiane…samahani Kwa mashabiki zangu ninaowakwaza Kwa hili. ☺#LINDALIPO TENA LA ZIGZAG HAHAHA HAHAHA,” 
Licha ya wawili hawa kuendelea kulumbana, Serikali kupitia Bodi ya Filamu imekanusha kuzuia ungizwaji, usambazaji na uuzaji wa filamu za kigeni nchini kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na vyombo vya habari. Bodi wamesema kuwa, wao wanasisitiza kuheshimu sheria na taratibu zilizopo katika bishara hiyo, ili serikali iweze kukusanya kodi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post