BONDIA NICOLA ADAMS AANZA NGUMI ZA KULIPWA KWA USHINDI

Mshindi wa medali mbili za dhahabu za Olimpiki mwanadada Nicola Adams amecheza mchezo wake wa kwanza wa ngumi za kulipwa na kuanza kwa ushindi.

Adams mwenye umri wa miaka 34 amepata ushindi wa pointi 40-36 dhidi ya Muargentina Virginia Carcamo katika pambano lililofanyika Jijini Manchester City.

Akiongelea pambano hilo Adams amesema hakutaka kumaliza pambano hilo mapema kwa kuwa alikuwa akitaka kutoa burudani kwa mashabiki wa ngumi.

Katika michezo ya ngumi za ridhaa Adams alishinda medali ya dhahabu Jijini London mwaka 2012 na Rio nchini Brazil mwaka 2016.
                                 Nicola Adams akimpa konde la kulia bondia Virginia Carcamo
                                Bondia Nicola Adams akiendelea kumuadhibu bondia Virginia Carcamo
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post