BREAKING NEWS: MBUNGE NAPE NNAUYE AITAJA SIKU NA MAHALI KUELEZEA UKWELI WOTE

Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kuwa Jumamosi April 8, 2017 atakuwa jimboni kwake ambapo atazungumza na wapiga kura wake kuwaeleza ukweli wa mambo yaote yaliyotokea.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Nape Nnauye amendika kuwa, “Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki. Narudi Mtama kuwaeleza wapiga kura wangu UKWELI WOTE. Ni Jmosi hii tar 8/4/17.”
Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki. Narudi Mtama kuwaeleza wapiga kura wangu UKWELI WOTE. Ni Jmosi hii tar 8/4/17.
Kauli hii ya Nape Nnauye imekuja ikiwa ni wiki mbili sasa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli alipotengua uteuzi wake kama Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Nape aliiongoza wizara hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja, na uteuzi wake ulitenguliwa Machi 23 mwaka huu ikiwa nu siku moja baada ya kukabidhiwa ripoti kuhusu uvamizi wa ofisi za Clouds Media Group tukio ambalo linadaiwa kufanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post