BREAKING NEWS : ROMA MKATOLIKI NA WENZAKE WAPATIKANA WAKIWA HAI

Saa chache baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro kuwaambia waandishi wa habari kuwa hawezi kusema ni lini mwanamuziki  Roma na wenzake watapatikana, taarifa kutoka kwa mmiliki wa studio walipokamatiwa, amethibitisha kuwa wamepatikana.
J Murder ambaye ndiye mmiliki wa Tongwe Records walipokuwa Roma na wenzake kabla ya kukamatwa na watu wasiojulikana, amesema kuwa wasanii hao wamepatikana na wapo katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Hakuna taarifa yoyote iliyoeleza wasanii hao wamepatikana wapi au ni nani aliyekuwa anawashikilia na sababu hasa za kufanya hivyo ni zipi.
Roma na wenzake watatu walikamatwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia Jumatano ambapo mbali na wao kuchukuliwa, watu hao pia walichukua baadhi ya vifaa vinavyotumika studio bila kueleza sababu za kufanya hivyo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post