BREAKING: TRA WAKAMATA BASI LA SERENGETI BOYS LIKIELEKEA KWA MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU

DAR ES SALAAM: Mamlaka  ya Mapato Tanzania (TRA) wamelikamata basi la timu ya Taifa vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) walilokuwa wakilitumia kwenda nyumbani kwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu kwa ajili ya chakula cha usiku.
TRA wamekamata basi hilo kupitia kwa Kampuni ya Udalali ya YONO ambapo basi hilo linamilikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).
Basi hilo ni la timu ya taifa ya Tanzania lakini kwa sasa linatumiwa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.
Gari limechukuliwa katika Hotel ya Urban Rose likiwa linawasubiri wachezaji wa Serengeti Boys liwapeleke kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu.
Sababu ya kukamatwa kwa basi hilo ni deni la kodi ya mapato ambayo TFF inadaiwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post