BREAKING: WATU WALIOVALIA VINYAGO WAKIWA NA BASTOLA WAVAMIA MKUTANO WA MAALIM SEIF

Watu wasiofahamika wakiwa na silaha za moto wamevamia mkutano wa wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) upande unaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo uliokuwa umepangwa kufanyika katika Hoteli ya Vina, Mabibo ulitarajiwa kuanza saa tano asubuhi lakini kabla haujaanza watu waliovalia vinyago vyeusi usoni (masks) walivamia na kuanza kuwapiga wanachama wa CUF na waandishi waliokuwa kwenye mkutano huo.
Mtu mmoja miongoni mwa wavamizi wa mkutano huo ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka. Haikufahamika mara moja jina lake na wametokea wapi, au lengo lao hasa la kutekeleza vurugu hizo.

Lakini pia haijafahamika bado kama kuna watu waliojeruhiwa kutokana na uvamizi huo, au hasara nyingine iliyosababishwa na tukio hilo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post