BUNGENI: SPIKA WA BUNGE AAGIZA HALIMA MDEE AKAMATWE NA POLISI POPOTE ALIPO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (Mb) ametoa saa 24 kwa Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee kujisalimisha mwenyewe bungeni au apelekwe na Polisi.
Spika Ndugai ameyasema hayo leo ikiwa ni kikao cha tatu cha mkutano wa saba wa bunge la 11 ambapo alikuwa akizungumzia suala la maadili ya wabunge wanapokuwa ndani ya bunge.
Spika amemtaka Mbunge Halima Mdee ambaye hayupo Dodoma, hadi kesho asubuhi awe amefika bungeni au vinginevyo akamatwe na Polisi popote pale alipo na apelekwe akiwa amefungwa pingu. Amri hiyo ya Spika imekuja kufuatia tuhuma zinazomkabili mbunge huyo kuwa alimtukana Spika katika moja ya vikao vya bunge hilo.
Mbali na Mdee, Spika amemuagiza pia Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Mb) kufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Kinga, Maadili na Madaraka leo akituhumiwa kulitukana bunge baada ya wagombea wawili wa CHADEMA kushindwa katika uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika Aprili 4 mwaka huu.
Mwingine anayetarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Kinga, Maadili na Madaraka leo ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Pastory Mnyeti ambaye ameitwa na kamati hiyo leo na anatakiwa kufika leo.

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post