CCM YATOA POLE KWA RAIS DKT.MAGUFULI KUFUATIA VIFO VYA ASKARI NANE

Chama cha Mapinduzi CCM kimetoa salamu za pole kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Dkt. John Pombe Magufuli kufuatia kuuwawa kwa askari polisi nane  kwa kushambuliwa na watu wenye silaha katika eneo la Jaribu Mpakani ,Wilaya ya kibiti mkoani Pwani.
Salamu hizo zimewasilishwa kwa Rais Magufuli na Katibu wa NEC  Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Akiwa ameambatana na Naibu Katibu Kuu CCM Tanzania Bara Rodrick Mpogolo na Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Bi Amina Makilagi,   Ndugu Polepole amesema kwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM ndio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, hivyo ndio maana CCM imeshtushwa na tukio hilo na kutoa pole hizo kutokana na kuuwawa kwa askari hao ambao wamekuwa na jukumu kubwa la kulinda usalama wa wananchi na mali zao .
Amesema askari hao wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu wakati wote kuhakikisha watanzania wanakuwa salama pamoja na mali zao hivyo tukio la kuuwawa kwao ni jambo la kusikitisha sana.
Pia Polepole amesema wamekutana na Mheshimiwa Rais kumueleza mchakato wa Uchaguzi wa ndani wa CCM ambao unaendelea nchini kote kuanzia ngazi ya mashina hadi taifa.
Aidha amesema CCM inampongeza Rais Dkt.Magufuli kwa kitendo cha kizalendo cha serikali ya awamu ya tano  kutumia fedha zake za ndani katika ujenzi wa Reli itakayokuwa na kiwango cha kimataifa yenye urefu wa kilomita 300 kutoka Dar es salaam hadi Morogoro.
Amesema ujenzi wa reli hiyo yenye kiwango cha kimataifa itakayotumia treni ya umeme inadhihirisha jinsi CCm inavyojishughulisha na shida za watu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post