CELTA VIGO YATUMIA VYEMA UWANJA WAO WA NYUMBANI NA KUWAFUNGA WAKINA SAMATTA

Iago Aspas ameendelea kufanya vizuri katika ufungaji wakati Celta Vigo ikiwazamisha wakina Mbwana Samatta na timu yake ya KRC Genk kwa magoli 3-2 katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Uropa uliochezwa Hispania.

Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool amefunga goli lake la 22 katika kampeni ya kukisaidia kikosi cha Eduardo Berizzo kupata goli moja muhimu la ziada dhidi ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Celta Vigo iliutawala mchezo huo katika muda mwingi lakini walikuwa wageni KRC Genk ambao walianza kufunga goli kupitia kwa Jean-Paul Boetius katika dakika ya 10 tu ya mchezo huo.
                               Iago Aspas akijipinda kuachia shuti lililojaa wavuni na kufunga goli
                       Kiungo Pablo Hernandez akiruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post