CHELSEA YAICHAPA BOURNEMOUTH NA KUENDELEA KUJIKITA KILELENI

Chelsea imeendelea kuongoza Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi saba, kwa kupata ushindi murwa wa magoli 3-1 dhidi ya Bournemouth.

Ikiwa na shinikizo la Tottenham ambayo iliifunga mapema Watford, wageni Chelsea walionekana kuanza vyema mchezo huo baada ya kupata magoli mawili kipindi cha kwanza.

Hata hivyo Bournemouth, ambao waligonga mwamba wa goli, walichomoa goli moja kupitia shuti la mpira wa mbali la Joshua King.

Bournemouth waliaendelea kufanya mashambulizi, lakini walikuwa Chelsea waliobahatika kufunga goli la tatu kupitia mpira wa adhabu uliopigwa kiufundi na Marcos Alonso.
   Diego Costa akishangilia baada ya mpira alioupiga kutumbukizwa kimiani na Adam Smith aliyejifunga 
                    Eden Hazard akiwa ametumbukiza kimiani mpira na kuandika goli la pili 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post