CRISTIANO RONALDO ARUDISHA MAKALI YAKE KATIKA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Cristiano Ronaldo amemaliza kwa kishindo ukame wa kutofunga magoli kwa miezi sita katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Real Madrid ikitokea nyuma na kuifunga Bayern Munich magoli 2-1.

Ronaldo, ambaye anashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, alifunga mara mbili, katika kipindi cha pili na kumaliza ukame wa saa 11 bila kufunga goli katika ligi hiyo.

Bayern Munich walikuwa wa kwanza kufunga goli kupitia kwa Arturo Vidal, lakini baadaye alipoteza nafasi nyingi za kuongeza goli la pili ikiwa ni pamoja na kupiga penati iliyotoka nje ya goli.
                                                  Arturo Vidal akifunga goli pekee la Bayern Munich

                     Cristiano Ronaldo akinyanyua mkono juu kushangilia goli alilofunga
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post