GHANA YAVUNJA REKODI KWA KUWA NA MEZA NDEFU ZAIDI DUNIANI

Bidhaa ya chakula inayoongoza sana katika soko nchini Ghana ya ONGA imevunja rekodi ya dunia ya Guinness kwa kuandaa na meza ndefu zaidi ya karamu.
Hii imeifanya kampuni ya Promasidor Ghana Limited watengenezaji wa ONGA kuwa kampuni ya kwanza nchini Ghana kuvunja rekodi hiyo ya dunia ya Guinness.
Meza hiyo ilikuwa na urefu wa mita 1,928 na iliandaliwa na Onga Ghana siku ya maadhimisho ya uhuru mjini Accra mnamo Machi 25, 2017.
Onga waliiandaa meza hiyo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano ya bidhaa hiyo, ambapo waliwakaribisha wapishi mbalimbali kuandaa chakula kwa ajili ya watu watakaohudumiwa katika meza hiyo.
Ushindi huo umepatikana baada ya kuishinda rekodi ya dunia iliyokuwa imewekwa nchini saudi Arabia iliyokuwa na meza ya urefu wa mita 1,508 iliyowahudumia wageni 3000 kwa vyakula vya asili na burudani mbalimbali.
Akiongea katika uwanja wa Uhuru wa Accra, Mkurugenzi wa Promisador Ghana Ltd, Dirk Laeremans alisema kuwa tukio hilo lililenga kuonyesha utajiri wa vyakula vya kiasili vya nchi hiyo hasa kwa kuwa walikuwa wanaadhimisha miaka 60 ya uhuru.
“Lengo letu halikuwa tu kuivunja rekodi ya dunia ya Guinness ila pia ni kuuonyesha ulimwengu utajiri wa vyakula uliopo Ghana.”
Meza hiyo ya Onga imeizidi urefu ile ya Saudi Arabia kwa mita 400
Hapa Chini ni video inayoonyesha meza hiyo ya ONGAJIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post