HATUA TATU ZILIZOCHUKULIWA KUPUNGUZA MADARAKA YA MWALIMU NYERERE

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Aidan Kabuni wakati wa kujibu hoja zilizotolewa na wabunge baada ya kuwasilisha bajeti ya makadirio ya matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2017/18, aliamua kuligeuza bunge kuwa chumba cha darasa na kuanza kuwalezea wabunge masuala mbalimbali ya kisheria.
Waziri Prof. Kabudi ni mbobezi katika masuala ya sheria na kabla ya kuteuliwa na Rais kuwa mbunge na kisha kuwa waziri, alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Kitivo cha Sheria.
Miongoni mwa mambo mengi aliyoyachambua Prof. Kabudi ni namna madaraka ya Mwalimu Nyerere yalivyopunguzwa kabla ya kung’atuka madarakani.
Prof. Kabuni alisema kuwa, wakati Mwalimu Nyerere anaelekea kutoka madarakani mwaka 1985 alisema kuwa ni lazima madaraka ya rais yapunguzwe kwani katiba ilikuwa imempa rais wa nchi mamlaka makubwa sana kiasi cha kuonekana kama Mungu mtu. Mambo matatu yalifanyika kupunguza mamlaka ya Rais, wakati huo;
Moja, kuanzisha cheo cha Waziri Mkuu. Hii ilikuwa ni njia moja wapo ya kupunguza mamlaka ya Rais ambapo cheo cha Waziri Mkuu ambaye ndiye msimamizi wa shughuli za kila siku za serikali kilianzishwa.
Mfumo wa kumpata Waziri Mkuu wa Tanzania si sawa na ule wa Uingereza bali ni kama wa Ufaransa ambapo Waziri Mkuu hutokana na chama chenye wabunge wengi bungeni wa kinachoungwa mkono na wabunge wengi.
Waziri Mkuu wa Tanzania hupatikana kwa kupigiwa kura na wabunge kama anakubalika baada ya kuwa amependekezwa na Rais.
Pili, hatua ya pili ilichokuliwa kupunguza madaraka ya rais ilikuwa ni kuweka ukomo wa uongozi.
Mwalimu Nyerere aliongoza kwa kipindi cha miaka 23 tangu Tanzania (Tanganyika wakati huo) lakini ili kudhibiti hali hiyo kujirudia ukomo wa madaraka uliwekwa ambapo Rais angeweza kuongoza kwa vipindi viwili vya hadi miaka 10 na baada ya hapo anatakiwa kuachia madaraka.
Kwa mujibu wa Prof. Kabudi, Tanzania ndiyo nchi ya kwanza barani Afrika kuweka ukomo wa madaraka ya rais ikifuatiwa na Senegali baada ya Rais wao wa kwanza kung’atuka.
Hatua ya tatu iliyochukuliwa kudhibiti madaraka ya Rais ilikuwa ni, kujumuisha sura ya haki za binadamu katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya mabadiliko hayo, ibara ya 12 hadi 29 zinazozungumzia masuala ya haki za binadamu hazikuwepo. Sura za haki za binadamu, zilijumuishwa katika katiba ili kudhibiti vitendo vya rais anavyoweza kufanya juu ya raia ikiwa ni pamoja na kuzuia raia kujieleza, kukusanyika.
Aidha, Prof. Kabudi katika kuonyesha ukomavu wake katika sheria amesema kuwa, akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alianzisha programu ya “Legal History” (Historia ya Sheria) akiwa na lengo la kufundisha historia ya sheria ya Tanzania kwani aliona vijana wengi hawaijui historia hiyo, wakidhani kuwa hali ilivyo sasa, ndivyo ilivyokuwa awali.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post