HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU TANZANIA BARA WIKI HII

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kuanzia Alhamisi wiki hii ambako katika mechi zote saba zitakazochezwa, mchezo mmoja tu kati ya Ruvu Shooting na Majimaji utafanyika saa 8.00 mchana kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani ilihali mechi nyingine zitaanza saa 10.00 jioni.

Kwa mujibu wa ratiba, Alhamisi Aprili 13, 2017 timu ya Mbeya City itaikaribisha African Lyon ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni.
Jumamosi ya Aprili 15, mwaka huu kutakuwa na michezo minne ambako Stand United itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga wakati Toto Africans ya Mwanza itaialika Simba SC ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Mechi hizi, zitachezwa kuanzia saa 10.00 jioni.
Kadhalika siku hiyo ya Jumamosi, Majimaji ya Songea itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani – mchezo utakaoanza saa 8.00 mchana ilihali JKT Ruvu ikiwa kwenye Uwanja wake mpya wa nyumbani – Mkwakwani jijini Tanga itaialika Azam ya Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni.
Jumapili Aprili 6, mwaka huu Mbao itacheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza huku Mwadui ikiwa mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Mwadui mkoani Shinyanga. Kadhalika, mechi hizo zitaanza saa 10.00 jioni.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post