HII NDIYO BEI YA PERFUME YA DIAMOND PLATNUMZ ILIYOZINDULIWA RASMI LEO

Leo Nasib Abdul maarufu kwa jina la sanaa Diamond Platnumz amepiga hatua nyingine mbele baada ya kufanikiwa kuzindua rasmi manukato yake yanayokwenda kwa jina la Chibu Perfume ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na Watanzania hasa mashabiki wake.
Diamond Platnumz leo mchana alikutana na kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi bidhaa hiyo ambapo amesema kwa sasa bidhaa hiyo itaanza kupatikana karibia mikoa yote hapa nchini na kwamba bado yuko kwenye utaratibu wa kuhakikisha anapata mawakala kila sehemu.
Akitaja bei ya manukato hayo, Diamond Platnumz amesema itapatikana kwa Tsh 105,000 (laki moja na elfu tano), bei ambayo anaamini si kubwa sana kwa watanzania walio wengi.
Uzinduzi huu wa Diamond ni hatua nyingine aliyopiga ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu alipozindua tovuti ya wasafi.com inayotumika kuuzia nyimbo za wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post