IDADI YA WAFUNGWA WALIOPEWA MSAMAHA NA RAIS MAGUFULI KATIKA SHEREHE ZA MUUNGANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 2,219 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Projest Rwegasira wafungwa hao ni wale wenye magonjwa kama UKIMWI, Saratani, Kifua Kikuu na wazee wenye umri wa kuanzia miaka 70.
“Ni mategemeo ya Serikali kwamba watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.” Imesema taarifa hiyo
Katika kuadhimisha miaka 53 ya Muungano,  sherehe hizo zimefanyika Makao Makuu ya Nchi, Dodoma ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Uamuzi huu umekuja ikiwa ni mpango wa serikali kuonyesha nia ya dhati ya kuhamia Dodoma kama ambavyo imekuwa ikielezwa na Rais Magufuli.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post