IFAHAMU AINA YA NGOZI YAKO NA JINSI YA KUITUNZA KUEPUKA MADHARA

Zipo ngozi za aina tofauti tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine. Wapo wenye ngozi kavu, zenye mafuta na wenye ngozi za kawaida.
Kujua aina ya ngozi yako kutakusaidia wewe kutafuta mbinu mbali mbali za kuifanya ngozi yako kuendelea kuwa bora na yenye muonekano wa kuvutia.
Wapo baadhi ya watu wenye ngozi ambazo siyo kavu wala siyo za mafuta sana na wala siyo za kawaida. Kwa mfano mtu kuwa na mafuta mengi katika eneo la paji la uso kupitia kwenye pua mpaka kidevuni huku mashavu ni makavu.
Aina za ngozi hutambuliwa kwa kupima kiwango cha mafuta kinachotengenezwa na ngozi. Kwa ngozi ya kawaida, kiwango fulani cha mafuta hutengenezwa na mwili ili kuifanya iwe nyororo wakati wote. Ngozi yenye mafuta mengi huwa ni pale ambapo mwili unatengeneza mafuta mengi kuliko kiwango cha kawaida.
Ngozi huwa haibaki katika hali moja wakati wote. hubadilika kulingana na hali ya hewa, umri, mabadiliko ya homoni mwilini pamoja na magonjwa. Hivyo ni vyema kuyatambua mabadiliko ya hali ya ngozi yako na sababu zake. Hii itakusaidia kujikinga dhidi ya madhara yanayoweza kukupata kupitia ngozi.
Siku hizi kuna aina nyingi ya bidhaa zinazotumiwa kuiweka ngozi yako katika hali nzuri. Bidhaa hizo zimetengenezwa tofauti tofauti na kwa matumizi tofauti kulingana na aina ya ngozi ya mtumiaji.
Hivyo wakati wa kuchagua bidhaa kwa ajili ya kuitunza ngozi yako, kuwa makini sana. Ijue aina ya ngozi yako, mafuta unayotakiwa kuyatumia na namna ya kuyatumia, usichague tu mafuta kwa kuwa yana jina kubwa.
Kwa kufanya hivi utakuwa na ngozi nyororo na yenye mvuto kila wakati.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post