IKUFIKUE HII KUTOKA FIFA KUHUSU UWANJA WA CCM KIRUMBA

Moja kati ya viwanja vyenye historia kubwa katika mchezo wa soka hapa kibongo bongo ni pamoja na uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza.
Unacotakiwa kukifahamu kama ulikuwa hujasanuka ni kwamba uwanja huo ulikuwa haujapewa ruhusa na mashirikisho ya mpira wamiguu barani Africa na Dunia yaani CAF na FIFA kwa kutumika katika michezo ya kimataifa.
Sasa good news ni kwamba CAF na FIFA wameupitisha uwanja huo na tayari kabisa kuanza kutumika kwa michezo ya kimataifa kama ulivyo uwanja wa Taifa uliopo Dar es Salaam.
Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi amedropisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kutoa hongera kwa wana Mwanza wote.

Wana Mwanza hongereni Uwanja wa CCM Kirumba umepitishwa na CAF na FIFA kutumiwa kwa mechi za Kimataifa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post