ISOME HAPA BARUA YA RAIS WA CHINA ALIYOMTUMIA RAIS MAGUFULI KUHUSU MUUNGANO

Kila tarehe 26 Aprili huwa tunaadhimisha kumbukumbu za sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizoungana Aprili 26, 1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina ambalo baadae lilibadilishwa mnamo tarehe 28 Oktoba, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.
Katika sherehe hizi, viongozi mbalimbali wa kimataifa, mashirika na watu maarufu hutuma salamu za pongeza kwa Tanzania kuendelea kuulinda muungano wake, ukiwa ni moja ya miungano michache iliyosalia dunia.
Hapa chini ni barua ya Rais wa China aliyomtumia Rais Dkt Magufuli;
Beijing,
Aprili 22, 2017.
Mheshimiwa Dr. John Pombe Magufuli,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Mheshimiwa,
Katika kuadhimisha miaka 53 ya kuasisiwa kwa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, kwa niaba ya watu wa China na kwa niaba yangu, napenda kuwapa pongezi za dhati na kuwatakia kila la kheri wewe na rafiki zetu wa Tanzania.
Miaka ya karibuni, urafiki wa kijadi kati ya China na Tanzania umekuwa uking’aa kwa nguvu mpya na imani yetu ya kisiasa kwa pamoja ikiendelea, ushirikiano baina ya nchi zetu katika nyanja zote ukizaa matunda tajiri na faida halisi ikiwasilishwa kwa watu wa pande hizi mbili.
Maendeleo ya Uhusiano kati ya China na Tanzania yana umuhimu mkubwa sana katika ajenda zangu. Ningependa tuunganishe juhudi zetu kwa pamoja ili kuelekeza nguvu katika kutekeleza ushirikiano wa kina wa China na Tanzania na kufanya ushirikiano baina ya China-Tanzania kukua kwa nguvu zaidi na haraka.
Naitakia Tanzania ustawi endelevu na mafanikio kwa watu wake yenye amani na furaha.
Xi Jiping,
Rais wa Jamhuri ya Watu wa China.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post