J MURDER AELEZA HATMA TONGWE RECORDS BAADA YA KUVAMIWA

Mkurugenzi wa studio za muziki za Tongwe Records zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam, J Murder leo amefunguka na kusema kuwa studio hizo zitafungwa kwa muda mpaka hapo hali za kiafya za wasanii waliotekwa wakiwa katika studio hiyo kukaa sawa.
Hii ni baada ya kupita kwa wiki kadhaa tokea msanii wa hip hop Ibrahim Mussa maarufu kama ‘Roma Mkatoliki’ pamoja na wenzake watatu, Moni, Imma na Bin Laden kutekwa wakiwa kwenye studio hizo na kupatikana baada ya siku tatu wakiwa na majeraha.
“Ni kweli Studio kwa sasa haifanyi kazi kwa sababu watu bado hawajakaa sawa, wanahitaji kupumzika kwanza,” alisema Murder.
“Mimi nadhani kwa sasa afya ya vijana wetu ndio kipaumbele cha kwanza, mambo yakitulia kila kitu kitakuwa wazi,” aliongeza
Tukio hilo la utekaji nyara lililowapata wasanii hao bado linafanyiwa uchunguzi na vyombo vya usalama nchini ili kubaini wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria.
Roma pamoja na wenzake bado wanaendelea kuuguza majeraha waliyoyapata huku wakingoja uchunguzi wa Polisi ukamilike.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post