JAMII YA AWALI YA DINOSAURS YAPATIKANA TANZANIA

Matokeo ya utafiti uliofanyika nchini Tanzania yameonyesha kuwa mojawapo ya jamii wa awali wa dinosaria (dinosaurs) alikuwa na maumbile yanayofananishwa na mamba.
Wataalam wa masuala ya uhifadhi wa mabaki ya wanyama wamekuwa wakijiuliza familia ya dinosari wa kitambo walifanana vipi, kwani maelezo ya rekodi kutoka enzi hizo ni nadra.
Wengine walidhania walitembea kwa miguu miwili, wakifanana kama dinosari wadogo.
Lakini matokeo ya utafiti huo yanaonyesha kuwa mnyama huyo alikuwa akitembea kwa miguu minne kama vile mamba.
Soma ripoti nzima hapa: Jarida la Nature
Mnyama huyo mla nyama mwenye urefu wa kati ya mita 2-3 aliyevumbuliwa Kusini mwa Tanzania aliishi takribani miaka milioni 245 iliyopita wakati wa kipindi cha kwanza cha maisha yao (Triassic).
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post