JB NA YUSUF MLELA WAMSHAMBULIA NAY WA MITEGO

Muigizaji wa filamu nchini Yusuph Mlela katika ukurasa wake wa instagram ameandika maneno yanayoonyesha kuwa alikasirishwa, kwa kile alichokieleza msanii wa muziki Nay wa mitego na kudai kuwa msanii huyo anapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya baadhi ya waigizaji wa filamu nchini.
Hii ni baada yakusambaa kwa video inayomwonyesha Msanii nay wa mitego akisema kuwa waigizaji hao walioandamana wana upungufu wa akili na kuwataka kutengeneza filamu zenye ubora ambazo zitauzika kirahisi kuliko kuandamana kuzuia filamu za nje kuuzwa nchini.

Kutokana na jambo hilo, ndipo hapo muigizaji Yusuph Mlela alipoamua kushusha ujumbe kwa msanii Nay wa Mitego


Yusuf Mlela amekwenda mbali zaidi na kutaka kuthibitisha kuwa yeye ni kinara kwa kuomba pambano la ndondi kati yake na Nay wa mitego ili ajulikane nani mwenye uwezo zaidi ya mwingine. Na ili kuonyesha kuwa anamaanisha alichokisema, Mlela ameweka video akiwa anafanya mazoezi kama ishara ya kujiandaa kwa pambano kati yao.


Mbali na Yusuf Mlela, Muigizaji nguli wa filamu nchini, Jacob Steven maarufu kama JB ameibuka kuweka sawa lengo la wao kuandamana kuwa wanataka filamu zinazoingizwa nchini zifuate utaratibu kama wanavyofuata wao wenyewe na siyo kuzuiliwa kwa filamu hizo.
“Ngoja tumalize hili tusichanganye na pia hakuna aliyesema zifungiwe hapana zifuate utaratibu kama sisi tunavyofuata hizo hizo ‘movie’ zetu mbovu ndiyo zinatuwezesha kuishi lakini pia lazima mfahamu biashara hii ni kubwa kuliko mnavyodhania, muvi mbili zinanitosha kuishi kwa mwaka mzima, ushawaza ni kiasi gani ?”. Alisisitizia JB
JB alikiri kwamba ni kweli filamu zao zina mapungufu mengi lakini isiwe sababu ya wao kuacha kudai haki zao wanazoamini kuwa wananyonywa katika pato la mauzo.
“Kwenye shida mimi sitajali nani ananisaidia ili mradi anagusa maslahi yangu, ugali wangu. Nakiri sinema zetu zina mapungufu mengi lakini hilo siyo sababu za kuacha kudai haki zetu, ni kama mgonjwa akiumwa leo anapelekwa kwa mganga kesho anapelekwa kuombewa, anatetea roho yake”. Aliongeza
Pia kupitia ukurasa wake wa instagram aliandika hiviJIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post