JINA "DAUDI BASHITE" LAZUA BALAA KWA WABUNGE WA CCM

Wabunge wa CCM wameitaka Serikali kutoa majibu sahihi bungeni kuhusu utambulisho wa mtu aitwaye Daudi Bashite.
Sakata hilo liliibuka juzi katika kikao cha wabunge wa CCM kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Dodoma.

Wabunge tofauti waliozungumza na Mwananchi walisema kuwa, suala hilo lilihojiwa kwenye kikao hicho cha ndani ambacho hufanyika kabla ya mkutano wa Bunge kwa ajili ya kuwekana sawa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wabunge hao walidai kuwa Serikali imeendesha na inaendelea kuhakiki vyeti vya elimu na baadhi ya watumishi wameshakumbwa na adhabu au kufukuzwa kazi kwa tatizo la vyeti feki.
Mpashaji mwingine aliiambia Mwananchi kuwa, Waziri Mkuu alijibu kuwa Serikali imepokea hoja hiyo bila kutoa ufafanuzi zaidi.
Pamoja na kelele za watu tofauti kueleza uwezekano wa kughushi vyetu, si Baraza la Mitihani (Necta), Polisi wala Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iliyojitokeza kuzungumzia suala hilo au kuchukua hatua 
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post