JOKATE MWEGELO ATEULIWA KUWA BALOZI MWEMA WA KUJITOLEA

Mrembo na Mjasiriamali Jokate Mwegelo leo ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kuwa Balozi Mwema wa Kijitolea wa mchezo huo akiwa nje na ndani ya nchi.
TBF imeeleza kuwa, lengo la uteuzi huo ni kusaidia kuwashawishi vijana kushiriki katika michezo hasa mchezo wa Mpira wa Kikapu. Ushiriki wa vijana katika michezo utawasaidia katika masomo yao, kuwawezesha kuwa na afya bora na pia kuwa na nidhamu na wazalendo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jokate Mwegelo ameandika ujumbe huu baada ya kupokea barua hiyo;
Nimepokea barua kutoka Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania kwa kunichagua kama Balozi Mwema Wa Kujitolea – Mpira wa kikapu niwapo ndani na nje ya nchi. Na kusaidia kuhamasisha mchezo huu hasa kwa upande wa watoto wa kike.
Kiukweli nimefarijika sana kwanza kwa kutambua mchezo wangu na nawashukuru sana sambamba na kuwaahidi sitowaangusha kwenye hili maana hii ni chaguzi kubwa hivyo heshima ni lazima iwepo katika kuitumikia. Uchapakazi ndio sifa yangu kuu, nitafanya kazi hii kwa nguvu zangu zote kuhakikisha Mpira wa Kikapu Tanzania unakuwa na kufikia ngazi za juu huku tukishirikiana na wadau wa michezo ndani na nje ya nchi ambao tayari wanafanya kazi kubwa tu na nzuri.
Na kwa kuanzia tu, tuna mpango wa kujenga viwanja vitano kwa mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwenye shule mbalimbali na kisha kuendelea katika miji mingine kama njia ya kutoa hamasa juu ya mchezo huu.
Nawakaribisha wadau wote kuchangia kwenye Harambee hii ya kujenga viwanja hivi ili kuboresha maeneo ya shule lakini vile vile kutoa hamasa kwa watoto kushiriki katika michezo mbalimbali na kutumia fursa hizi za michezo vizuri. #GoodwillBasketballAmbassador#Tanzania
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post