JUX AZUNGUMZA KUHUSU KUACHANA NA VANESSA MDEE

2Msanii Juma Jux maarufu kwa jina la Jux ambaye anatoka kimapenzi na msanii Vanessa Mdee maarufu pia kwa jina la Vee Money au Cash Madame amefunguka na kusema kwa sasa yeye hayupo ‘single’ kama ambavyo watu wanakuwa wakisema lakini pia amekanusha zile tetesi kuwa ameachana na mpenzi wake Vanessa Mdee.
Jux alisema hayo alipokuwa katika kipindi cha Friday Night Live cha EATV ambapo alifunguka kuwa taarifa ambazo zinasambazwa kuwa sasa yupo single si kweli japo alishindwa kunyoosha maelezo kama ni kweli ameachana na Vanessa au bado wapo pamoja.
“Naanza kabisa hiyo habari si ya kweli sasa kama habari si ya ukweli unadhani hapo ukweli ni upi? Si kila kitu unachokiona au kukisikia ni cha ukweli, sihitaji kuzungumzia suala hilo la Vanessa kwa sasa, lakini hiyo habari si ya kweli saizi mimi vitu vingi nimebadilika, hivyo nina kila uhuru wa kusema kwa hiyo kwanza nakusahihisha ile stori siyo ya kweli mimi siyo ‘single boy’ kwa hiyo kama ikiendelea hiyo habari iendelee lakini mimi nathibitisha kuwa hiyo habari si ya kweli” alisema Jux.
Mbali na hilo Jux alipatwa na kigugumizi kujibu swali moja kuhusiana na Vanessa Mdee, baada ya mtangazaji kumuuliza kama anaendelea kutoka na Vanessa, Jux alipojibu swali hilo alisema hayo ni mambo yake binafsi.
Wanamuziki hao wawili wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu sasa, lakini kwa siku za hivi karibuni kumekuwapo tetesi kuwa wamemwagana.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post