KADA WA CCM ALIYEFUKUZWA UANACHAMA, AKAMATWA NA POLISI

Jeshi la Polisi linamshikilia Jesca Msambatavangu, aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoani hapa kwa tuhuma za kuhusika katika shambulio dhidi ya mwanamke mmoja na kumjeruhi.
Hata hivyo, jeshi hilo halijafahamu sababu za shambulio hilo.
Msabatavangu, ambaye alipoteza uenyekiti baada ya kuvuliwa uanachama na Hlmashauri Kuu ya CCM, alikamatwa jana jioni.
Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Julius Mjengi alisema kuwa Msambatavangu alitenda kosa hilo wiki iliyopita. Alisema alifanya kosa hilo akiwa na wenzake ambao alisema hawataji majina kwa kuwa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.
“Ni kweli tunamshikilia Jesca Msabatavangu. tumemkamata leo saa 8:00 mchana na tunaendelea na uchunguzi dhidi yake. Jesca pamoja na wenzake wanatuhumiwa kumshambulia mwanamke mmoja mkazi wa Kibwabwa. Walimshambulia na kisha kumchoma sindano ambayo mwanamke huyo hajui ni ya kitu gani:” alisema Mjegi.
Mjegi alisema hawezi kuweka wazi jina la mwanamke huyo wala idadi ya watuhumiwa wengine kwa kuwa jambo hilo bado linachunguzwa.
Msambatavangu alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa hadi Machi mwaka huu wakati Halmashauri Kuu ilipofikia uamuzi wa kumvua uanachama kwa tuhuma za kukiuka kanuni za maadili ya CCM wakati wa uchaguzi.
Mara baada ya kufukuzwa uongozi, Jesca alitangaza kutojihusisha tena na shughuli zozote za siasa kwa kuwa yote yaliyotendeka ndani ya chama chake, amemwachia Mungu.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post