KAMPUNI YA BIA (TBL) YAWAFUTA KAZI WAFANYAKAZI 100 NDANI YA SAA 24

Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) imewafuta kazi takribani watumishi wake 100 ndani ya saa 24. Kwa mijibu wa taarifa iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania la Aprili 29, wafanyakazi waliopunguzwa ni wale wa kitengo cha masoko.
Mtoa taarifa kutoka ndani ya kampuni hiyo amesema kuwa hatua hiyo imetekelezwa siku ya Jumatatu ya wiki hii. Akielezea kusudi la kupunguza wafanyakazi, alisema kuwa ni kulinda uchumi wa kampuni kutokana na mauzo ya bidhaa kupungua kwa kasi tangu kipindi cha mwaka jana hadi mwaka huu.
Afisa wa masoko ambaye yeye hakukumbwa na panga la kupunguza wafanyakazi amesema kuwa, mauzo ya bidhaa kwa siku za hivi karibuni yamekuwa si rafiki sana, na pia uamuzi wa serikali kuzuia pombe zinazowekwa kwenye vifungashio vya plastiki kumeathiri kwa kiasi kikubwa mauzo ya pombe ya konyagi.
“Waliachishwa kinyama sana, waliitwa siku ya Jumatatu na kuachishwa hapo hapo, wakaambiwa wayaache magari na kusaini fomu ya kuondoka. Mie bahati nzuri nimepona, na hili jambo la viroba ndio limepigilia msumari wa mwisho” alisema afisa huyo.
Kwa mujibu wa Mtanzania, alipotafutwa Msemaji wa TBL, Georgia Mutagahwa kuweza kuthibitisha taarifa hizo hakupokea simu yake, akaomba kuandikiwa ujumbe mfupi kwa madai ametingwa na majukumu. Alipoandikiwa ujumbe hakujibu, na hata alipopigiwa tena hakupokea.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post