KAULI YA KWANZA NA MZEE MZINDAKAYA BAADA YA KUZUSHIWA KIFO

Mwanasiasa mkongwe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga mkoani Rukwa, Chrisant Majiyatanga Mzindakaya amekanusha taarifa zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa amefariki.
Taarifa zilizoanza kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii leo, zilidai kuwa Mzee Mzindakaya amefariki dunia. Mwanasiasa huyo amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa yeye ni mzima wa afya.
Mzindakaya amesema kuwa hatowashtaki wale wote walioshiriki kusambaza taarifa kuwa amefariki dunia lakini amewashauri kuwa wajikite zaidi kushughulikia afya zao badala ya kukaa tu kwenye mitandao na kuzusha habari.
Mapema leo asubuhi Mbunge wa Chalinze mkoani Pwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete alichapisha picha kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa na Mzee Mzindakaya alipomtembelea kumjulia hali. Ridhiwani alisema kuwa amefurahi kuona afya ya kiongozi huyo inazidi kuimarika.
“Nimekuja kumuona mzee wangu Mzee Mzindakaya. Furaha yangu ni kumuona afya yake inaendelea kuwa njema zaidi.”


Mzee Mzindakaya kwa sasa amelezwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ( JKCI) ambapo afya yake amesema inaendelea vizuri na amepatiwa huduma bora sana.
Alifikishwa hospitalini hapo siku ya Jumapili akitokea Mbeya ambapo amsema kuwa Malaria ndiyo ilikuwa ikimsumbua zaidi. Aidha amesisitiza kwa sasa moyo wake na figo zipo sawa na hata akiugua tena angependa atibiwe JKCI badala ya kupelekwa nje ya nchi kama ilivyokuwa awali.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post