KAULI YA WAZIRI WA ELIMU KUHUSU WAFANYAKAZI KUKATWA MKOPO 15% BADALA YA 8%

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa serikali haijakiuka makubaliano yoyote ya kisheria kwa kuongeza makato katika maishara ya watumishi walionufaika na mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Waziri Ndalichako aliliambia Bunge kuwa, hatua za kuongeza makato kwa walionufaika na mikopo kutoka asilimia 8 hadi asilimia 15 zilifanywa kwa uwazi mkubwa na kuwashirikisha wadau mbalimbali.
Kauli hiyo ya Waziri wa Elimu ilikuja wakati akijibu swali la Mbunge wa Kaliua, Magadalena Sakaya alipokuwa akihoji kwamba, wanufaikaji wa mikopo waliingia makubaliano na Bodi ya Mikopo ya kukatwa asilimia 8 ya mishahara yao, lakini kiwango hicho sasa kimepandishwa hadi asilimia 15 tena bila ridhaa yao. Itakuwa ni jambo jema na lenye manufaa hasa wa walimu wetu kama serikali itaamua kukata kiwango cha asilimia 8 walichokubaliana, alisema Sakaya.
Waziri alikanusha kuwa, mabadiliko hayo yalifanywa kwa siri akikumbushia kuwa muswada wa mabadiliko ya sheria ya HESLB ulipelekwa bungeni na wabunge wakaupitisha ukionyesha kuwa makato yatakuwa asilimia 15.
Maelezo haya ya waziri yamekuja majuma machache tu tangu Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kusema kuwa wataishtaki serikali mahakamani kwa kukiuka makubaliano ya kukata asilimia 15 badala ya asilimia 8 iliyokuwa kwenye mkataba wakati wa kuomba mkopo.
Kwa upande mwingine TUCTA wamesema kuwa walionufaika na mkopo huo hawakuhusishwa kwenye mabadiliko hayo, hivyo wataiomba mahakama iondoe mabadiliko hayo, na kama serikali itataka kuyarudisha, iwahusishe wanufaikaji wa mikopo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post