KAULI ZA VIONGOZI MBALIMBALI KUHUSU MAUAJI YA ASKARI POLISI 8 MKOANI PWANI

Viongozi mbalimbali wamezungumzia suala la mauaji ya Askari Polisi 8 yaliyotokea juzi jioni walipokuwa wakitoka kuweka doria katika eneo maalumu mkoani Pwani ambalo kwa muda sasa limekua na vitendo vingi vya kiuhalifu.
Hapa chini ni kauli za viongozi mbalimbali walizozitoa kuhusu tukio hilo lililoacha simanzi kubwa nchini.
"Bunga massacre" Kama Taifa tuungane kuwapa pole Jeshi la polisi na Familia za Askari walopoteza uhai wakitimiza wajibu wao wa kulinda Raia
Nyakati hizi zinatuleta kuwa wamoja zaidi tukiombeleza vifo vya askari wetu
Vijana 8 wa Jeshi la Polisi wameuwawa kikatili. Hatutaogopa na tuko pamoja nawe AmiriJeshi Mkuu. Ni desturi yetu kushinda. 
Saddened by the loss of police officers following an attack by unknown group terrorizing Coast region of Tanzania tonight 
Times like these require the nation to be together. We mourn our men in uniforms and send condolences to families. 
Tanzanians are at best when calm and UNITED. I hope CiC leads the nation to end these barbaric actions we vehemently condemn 

“Hatukubaliani, na jambo hilo halina nafasi. Mkuu wa Mkoa pokeeni pole, fungeni mkanda upya ili tuunganishe nguvu kukabiliana na uhalifu huu,” Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Lameck Nchemba.
“Hatuwezi kuishi kwa amani bila kuwa na Jeshi la Polisi imara na ili tuwe na Jeshi imara tunapaswa kuwa na jamii inayotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi hasa kwenye nyakati ngumu kama hizi,” Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema
“Tumekwisha kupoteza askari zaidi ya 10, ninaamini wanatosha sasa tunakwenda kwenye operesheni maalum, hatutakuwa na msamaha wala mzaha. Tutawapata popote walipo, tutawashughulikia kikamilifu hakuna atakayebaki, mapambano haya hayana mwisho, huu ni mwanzo usio na mwisho,” Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Marijani

“Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya askari wetu 8 ambao wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia Taifa, naungana na familia za marehemu wote, Jeshi la Polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu. “Namuomba Mwenyezi Mungu atupe moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post