KENYA: MCHEKESHAJI MAARUFU WA KIPINDI CHA CHURCHILL (CHURCHILL SHOW) AFARIKI DUNIA

KENYA: Tasnia wa vichekesho na sanaa kwa ujumla nchini Kenya na Afrika Mashariki wanaomboleza kifo cha mmoja wa wasanii wa vichekesho aliyefariki katika ajali ya gari usiku wa kuamkia leo Aprili 14 nchini humo.
Mchekeshaji Emmanuel Makori Nyambane a.k.a Ayeiya Poa Poa aliyekuwa akifanya kazi katika kipindi cha Churchill amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo.
The late Ayeiya poa poa
Mchekeshaji huyo alikuwapo kwenye gari pamoja na mkewe, muigizaji Maina Olwenya, mchekeshaji Paul Wakimani Ogutu na rafiki mwingine.
Ayeiya Poa Poa alifariki katika eneo la tukio lakini mkewe na Wakimani wamelazwa katika Hospitali ya Taifa.
Ajali ilitokea eneo la Catholic University of Eastern Africa (CUEA) na chanzo cha ajali kinadaiwa kuwa ni gari liligonga nguzo ya umeme.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post