KINDA KYLIAN MBAPPE ATUPIA MAWILI MONACO IKIIFUNGA BORUSSIA DORTMUND

Kinda Kylian Mbappe ametikisa nyavu mara mbili wakati Monaco wakipata ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Borussia Dortmund katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mchezo huo uliopaswa kuchezwa juzi lakini ukahairishwa baada ya tukio la milipuko, Mbappe alitumbukiza kimiani krosi ya Thomas Lemar kabla ya Sven Bender kujifunga na kuwa 2-0.

Ousmane Dembele alichomoa moja kupitia pande la Pierre-Emerick Aubameyang, lakini Mbappe tena akafunga goli la tatu kisha Shinji Kagawa akafunga goli la pili la Dortmund.
                                        Kylian Mbappe akifunga goli la kwanza katika mchezo huo

                                         Shinji Kagawa akifunga goli la pili la Borussia Dortmund
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post